Search This Blog

Thursday, April 22, 2010

SAVIO

SAVIO ni timu ya mpira wa kikapu ya Don Bosco Youth Center - Upanga, ambayo imeshinda kombe la NBL - National Basketball League mwaka huu na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Zone 5 yatakayofanyika huko Burundi mwezi wa nane kuanzia tarehe 9 hadi 15.

So wale wadau wa mpira wa kikapu muanze kuandaa safari ya kuelekea Burundi mwezi wa nane kushuhudia na kuwapa shavu wana wa SAVIO.


Hawa ni wana wa Savio Basketball Team kuanzia juu kushoto ni Dusa, Raza, Isiaka, Waziri, Abdul, Ally, Dassy, Maige, Jije, Joseph, George, Benard na Muddy. Vijana imara wanaoiwakilisha vizuri timu ya mpira wa kikapu ya SAVIO - the winning team with spirit of togetherness.



Pichani juu hapo SAVIO wakiwa katika mazoezi yao ya kujinoa vilivyo ili kurudi tena na kombe nyumbani hapo baadae mwezi wa nane mwaka huu wanapokwenda Burundi kuiwakilisha Tanzania katika michuano mikali ya basketball.


SAVIO baada ya kupokea kombe la NBL wakiwa na nyuso za furaha kabisa katika picha ya kumbukumbu na Kipingu (Wapili kutoka kulia)


SAVIO wakiwa Barbecue - Upanga.




No comments:

Post a Comment